Mchezaji wa klabu ya Wolfsburg afariki



Mchezaji Lukaku akimenyana na marehemu Junior Malanda.mchezaji huyo wa miaka 20 alifariki katika ajali ya gari huko Ujerumani
Mchezaji wa safu ya ulinzi ya katikati katika kilabu ya Wolfsburg nchini Ujerumani amefariki katika ajali ya barabarani.
Mchezaji huyo mwenye umri wa mika 20 aliripotiwa kukaa katika kiti cha nyuma cha gari kazkazini Magharibi mwa Ujerumani ambapo kulingana na maafisa wa polisi wa Ujerumani lilikuwa likipelekwa kwa mwendo wa kasi.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Bundesatobahn 2.
Malanda alitarajiwa kusafari hadi Afrika kusini na wenzake jioni ya leo kwa kambi ya mazoezi. 
CHANZO:BBC
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment