RONALDO AFANYA KUFURU YA PESA

Christiano Ronaldo (kulia) akiwa na Mendes mwaka 2009
Mkali wa soka wa klabu ya Real Madrid, mreno Chriastiano Ronaldo amemtunuku Jorge Mendes kisiwa kimoja cha Ugiriki kama zawadi yake ya harusi.
Kisiwa hicho hakijatajwa lakini thamani yake huenda ikawa ya mamilioni kulingana na ripoti hizo.
Kulingana na mtandao wa michezo wa Uhispania Mundo Deportivo,Ronaldo anakijua kisiwa hicho kutokana na ziara zake wakati wa likizo.
Bwana Mendes alimuoa mshirika wake Sandra nchini Ureno siku ya jumapili.
Alex Ferguson ni miongoni mwa wageni waliohudhuria harusi hiyo.
Mkufunzi huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United alimsajili Ronaldo mwaka 2003 na mshambuliaji huyo wa Ureno ambaye ni mmoja ya wachezaji bora duniani alihudumu katika kilabu hiyo ya Old Trafford hadi mwaka 2009.
Ronaldo ameshinda taji la Ballon d'Or kama mchezaji bora wa mwaka mara tatu.

BBC
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment