Mtanzania Diamond Platinumz awaacha midomo wazi wakenya

Diamond performs at the MTV After Party

Mshindi wa tuzo ya mtumbuizaji bora wa bara la Africa katika tuzo za MTV MAMA 2015, mtanzania Diamond Platinumz amedhihirisha ubora wake jukwaani katika tamasha la MAMA's After-party lilofanyika Jumamosi hii huko nchini Kenya.
Mamia ya mashabiki wa muziki waliohudhuria tamasha hilo walichizika kwa uwezo wa mkali huyo wa 'Nana'. Diamond alikuwa kivutio katika tamasha hilo lililogubikwa na wanamuziki maarufu wa nchini Kenya wakiwemo Nonini, Wahu, Nameless na Jaguar.
Watumbuizaji wengine katika tamasha hilo walikuwa ni Sauti Sol. Kundi hilo la muziki la Kenya lilitawala jukwaa likiwa kifua wazi huku wakitangaza ujio wa video yao mpya ndani ya muda wa wiki mbili zijazo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment