Baloteli kuisubiria Man U



Hatma ya Mario Baloteli katika klabu yake ya Liverpool imezidi kugubikwa na utata hasa baada ya kusajiliwa kwa mshambuliaji Christian Benteke ambaye anaonekana kuwa chaguo la kwanza kwa kocha Brendan Rogers. 

Hata hivyo mshambuliaji huyo mwenye sifa ya utukutu anaweza kuendelea kubaki kunako Ligi Kuu ya Uingereza na klabu ya Liverpool endapo Manchester United wataifunga na kuito klabu ya Lazio katika mtoano wa kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa Ulaya. Klabu hiyo ya Italia imepanga kumchukua Baloteli kwa mkopo endapo itafuzu hatua ya mtoano kwenda kwenye makundi kucheza klabu bingwa Ulaya (UEFA).

Man U watamtibulia ulaji Baloteli endapo wataitoa Lazio kwani Lazio imeshakubali kutoa Euro Milioni 12.5 kumsajili mshambuliaji huyo ili kukiongezea nguvu kikosi hicho cha Stefano Pioli kwenye michuano ya Ulaya.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment