Diamond na Davido wazidi kuchuana tuzo za kimataifa

Embedded image permalink
Mtanzania Diamond Platinumz ameendelea kuchanja mbuga kunako anga ya muziki wa kimataifa baada ya kuweza kuchaguliwa kuwania tuzo za MTVEMA katika nafasi ya Mwimbaji bora wa bara la Africa.

MTV EMA ni tuzo za muziki kwa bara la Ulaya. Katika kinyang'anyiro cha kuwania msanii bora wa Afrika Diamond anachuana na wakali wengine wa Afrika wakiwemo Wanigeria Davido na Yemi Alade na Mwafrika Kusini AKA. Hata hivyo bado una nafasi ya kumchagua msanii atakayekamilisha idadi ya wasanii kuwa watano katika kipengele hicho.Wasanii wanaochuana kumpata mmoja ni Mnigeria Wizkid, Wafrika Kusini Cassper Nyovest na KO, Mghana Stonebwoy na Mwaivory Cost DJ Arafat. Sherehe ya kutoa tuzo hizi itafanyika  Octba 25 huko Milan nchini Italia.
Muda wa kuanza kupiga kura ukifika tusisite kuileta heshima hii nyumbani Tanzania.
Share on Google Plus

About Mallya Michael

Born in Moshi ,live i Tanga, studied in Arusha, went for military training at Kanembwa in Kigoma & currently pursuing my B.A in Public Relations & Advertising in University of Dar es Salaam