DULLY SYKES: YAMOTO WAMENIANDIKIA WIMBO

Dully

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes.
MSANII mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes, amefichua siri kuwa wimbo wake mpya wa Tuachie umeandikiwa na vijana wa Kundi la Yamoto Band.

Dully amerejea tena kwa kasi baada kuachia video ya Wimbo wa Dodoma unaofanya vizuri kwa sasa pamoja na Tuachie aliowashirikisha Yamoto Band.
Akizungumza na Mikito Jumatano, Dully alisema amefurahishwa kwa jinsi mashabiki walivyompokea licha ya Wimbo wa Tuachie kuandikiwa na vijana hao wanaotamba na Wimbo wa Cheza kwa Madoido.
“Wimbo wa Dodoma nimeuimba kutokana na mawazo ya watu wangu wa karibu waliotaka niimbe kama zamani, ndiyo maana niliamua kujaribu vile ili nione kama inawezekana.
“Lakini kwenye Tuachie nimefurahi kuwashirikisha Yamoto Band kwa sababu wao ndiyo wameniandikia huo wimbo, ni kitu cha kawaida kutokea na uzuri wake mashabiki wangu wamezipokea vizuri,” alisema Dully.
Share on Google Plus

About Krantz Mwantepele

#IMAGINE #INSPIRE #INFLUENCE