SBL yakabidhi mradi wa maji wa thamani ya shilingi 80m/- kwa wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza



Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. Angelina Mabula (aliyevaa kofia) akikata utepe kuzindua kisima  cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh Milioni 80.

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh,Angelina Mabula,akifungua kitambaa cha jiwe la msingi la  kisima  cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion.

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula(aliyevaa kofia) akijaribu kumtiwhsa ndoo mara baada ya kuzindua kisima  cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion 

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. Angelina Mabula(wa pili kulia) na Meneja wa Kiwanda cha bia cha Serengeti Mwanza Shekhar Makasare, wakimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela jana,anayeshuhudia pembeni ni Meneja Uwajibikaji kwa jamii wa SBL Hawa Ladha, wakati wa uzinduzi kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh Milion 80 .




Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula,akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SBL Mwanza mara bada ya uzinduzi wa   kisima  cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion.


Meneja Uwajibikaji kwa jamii wa SBL Hawa Ladha, akizungumza na waandishi wa habari kijijini Maguha jana, wakati wa uzinduzi wa kisima,nkilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion

 Kisima,kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti ambacho kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.


Wananchi wakichota maji mara baada ya uzinduzi.

Wafanyakazi wa SBL Mwanza na wakazi wa Ilemela wakishuhudia hafla ya uzinduzi wa kisima hicho.

Mkazi wa Ilemela  akinywa maji kwenye ndoo mara baada ya uzinduzi wa kisima hicho.

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula(aliyevaa kofia) akicheza ngoma ya bugobogobo wakati wa  kuzindua kisima  cha kijiji cha Kaguha wilayani Ilemela mkoani Mwanza jana,alipozindua, kilichojengwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kitahudumia wakazi 7560 na kutoa lita 4000 kwa saa chenye thamani ya Sh 80Milion 


Wananchi wakitoka kuchota maji mara baada ya kuchota maji katika kisima kilichozinduliwa mapema jana

wakazi wa  kaguhwa Ilemela wakishangilia jambo wakazi wa Hafla ya uzinduzi wa kisima hicho mapema jana katika Jiji la Mwanza.



Kaguhwa Nyamhogolo Octoba 4, 2017 Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imekabidhi mradi wa maji safi wenye thamani ya shilingi milioni 80 kwa wakazi wa Kaghwa Nyamhogolo Wilayani Ilemela, Mkoani Mwanza.
Msaada huo ni sehemu ya jitihada za SBL kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama kwenye sehemu zenye uhitaji wa huduma hiyo muhimu. Ukiwa na uwezo wa kuhudumia watu 7,560, mradi huo unahusisha kisima, pampu ya maji pamoja na tanki lenye uwezo kuzalisha maji lita 4,000 kwa saa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi, Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL John Wanyancha alisema, mradi huo unaojulikana kama ‘Maji ni Uhai’ ni mmoja kati ya miradi ambayo SBL inaifadhili kwenye mikoa kama Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvunma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwezesha upatikanaji wa maji safi na salama kwa zaidi ya watu milioni moja.
Wanyancha alisema, mradi wa Kaghwa Nyamhogolo hautasaidia tu kuboresha afya za wakazi wa eneo hilo, bali pia utaongeza uzalishaji mali kwa kuwa wasichana na akina mama hawatatembea tena umbali mrefu kutafuta maji na kuongeza kuwa utawapa wasichana muda zaidi wa kuhudhuria shule.
SBL inayo sera inayolenga kuboresha maisha ya jamii zetu na Maji ni Uhai ni moja kati ya vipau mbele ambavyo vimeelezewa kwenye malengo ya kampuni yetu kuboresha maisha ya jamii inayotuzunguka,” alisemaWanyancha
Mkurugenzi huyo alitaja vipaumbele vingine kuwa ni pamoja na Kutoa ujuzi kwa ajili ya Maisha, Utunzaji wa Mazingira na Unywaji wa Kiasi.
Zaidi, Wanyancha alisema  SBL inao mpango wa kusaidia wakulima ambao kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita umefanikiwa kuwafikia na kuwasaidia wakulima 100 kwa kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha hivyo kuweza kuboresha maisha yao na ya jamii zao
“Kupitia mpango huu, SBL imeweza kupata malighafi kwa ajili ya uzalishaji wake kutoka tani 0 hadi 10,000 zinazozalishwa na wakulima wa ndani jambo ambalo limesaidia ukuwaji wa kampuni na kuongeza kipato kwa wakulima pia,” alisema.
“Ukiachana na kuchangia uchumi wa nchi kupitia ulipaji kodi, SBL inatoa mchango wake kwa maendeleo ya nchi haswa kwa kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama hapa nchini,” aliongeza
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni pia na Mbunge wa eneo hilo Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula aliishukuru SBL kwa msaada huo muhimu na uliokuwa unahitajika sana na kuongeza kuwa kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada ya kimaendele inayoigusa jamii

Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment