Alichokisema mke wa mchekeshaji Bill Cosby kuhusu tuhuma zinazomkabili mume wake


1416230085590_Image_galleryImage_Entertainer_Bill_Cosby_le
Habari ambazo zimetawala katika vyombo vya Habari takribani miezi miwili sasa kuhusu mchekeshaji maarufu Duniani Bill Cosby, baada wanawake kadhaa kujitokeza wakidai kuwa Cosby aliwadhalilisha kwa nyakati tofauti miaka ya nyuma.
Cosby hakuwahi kuzungumza chochote tangu madai hayo yaanze kuvuma, jana amezungumza kwa mara ya kwanza vyombo vya Habari kuzingatia usawa wakiwa wanaripoti kuhusu taarifa hiyo huku akimpongeza mke wake kwa kuwa karibu naye wakati wote tangu kuanza kwa matatizo hayo.
Mke wa Cosby, Camille amemtetea mume wake kwa kusema kuwa taswira ambayo imejengwa na vyombo vya habari kuhusu mume wake hajawahi kuiona kwa kipindi chote cha miaka zaidi ya 50 ambayo wamekuwa pamoja.
Camille amesema anampenda na ataendelea kumpenda Cosby licha ya taswira mbaya ambayo amejengewa mume wake huyo.
Bill Cosby anakabiliwa na shutuma za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na amekana kuhusika na vitendo hivyo na hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la kihalifu.
bill-cosby-1024
H
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment