Rapa Big Sean na mwanadada mkali wa Pop na R&B wamejibana sana katika kuonyesha mahusiano yao ya kimapenzi. Lakini kama wasemavyo waswahili, "mapenzi ni kikohozi" wawili hao wameshindwa kuvumilia na kuonyesha furaha yao ya kuwa pamoja baada ya hivi karibuni Big Sean kuweka picha katika mtandao wa Instagram ikimuonyesha yeye na Ariana wakiwa katika pozi la mahaba.
Kudhihirisha kuwa wawili hao wamezimikiana, siku moja kabla Ariana pia aliposti picha hiyo na kuandika maneno "happiest" akionyesha kuwa mapenzi yske na rapa huyo yamenoga kwelikweli.
Icheki post ya Big Sean hapa
0 comments:
Post a Comment