Idris Sultan "Licha Ya kushinda Zaidi Ya Milioni 500 Za BBA, Hiki Ndicho Kitu Sitobadilika..." Soma Hapa



Ni dhahiri kwamba ushindi wa Idris Sultan kwenye Big Brother Africa Hotshots umebadilisha mambo mengi katika maisha yake kwa muda mfupi, ikiwa ni pamoja na kumpa umaarufu sio tu Tanzania bali hata katika nchi nyingi za Afrika, umenenepesha akaunti yake kwa $300,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Tshs milioni 515 alizoshinda, lakini kuna kimoja ambacho amesema kwake hakitabadilika.

Idris (21) ambaye amerejea nyumbani Tanzania Dec.10 amesema ataendelea kuwa Idris yule yule. 

Alipoulizwa na Millard Ayo baada ya kutua uwanja wa ndege wa Dar es salaam kama ataendelea na kazi yake ya kupiga picha, hiki ndicho alichojibu:“Naendelea na kila kitu, mimi bado Idris tu vile vile sasa hivi am just enhanced nimekuwa mkubwa zaidi kwahiyo nategemea kufanya mambo makubwa zaidi .” Idris ni mpiga picha katika kampuni ya I-View Studios ya Dar es salaam.
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment