Divas wa Skylight Band wakitoa burudani kwa mashabiki wao Ijumaa iliyopita ndani ya viunga vya Thai Village Masaki wakiongozwa na Meneja wa Band Aneth Kushaba AK47 (katikati), Digna Mbepera (kulia) pamoja na Bela Kombo.
Aneth Kushaba AK47 sambamba na Bela Kombo wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam.
Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa bongo akifanya yake jukwaani kwa mashabiki wa Skylight Band huku akisindikizwa na Sam Mapenzi (kulia) pamoja na Joniko Flower.
Sam Mapenzi na Sony Masamba wakifanya ya jukwaani huku wakitega kwa ukodak.
Backstage nako walishindwa kujizuia nakuamua kupasha misuli moto huku wengine wakiendelea na kutoa burudani.
Diva Digna Mbepera akitoa burudani kwa wapenzi wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota Thai Village Masaki jijini Dar.
Bela Kombo katika hisia kali akiwapa raha wapenzi wa bendi ya Skylight Ijumaa iliyopita ndani ya viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
Aneth Kushaba na Sam Mapenzi kwenye Kolabo kali ya Utake (nyimbo za Afrika mashariki) huku wakisindikizwa na Digna Mbepera sambamba na Bela Kombo.
SAM MAPENZI;...Kuna Watu Hatari, Wenye Mapenzi Zenye Siri Kali,...Letu Nalo Lina Jua Kali, Penzi Letu Serikali,....Wajua Nakupenda, Malaika......ANETH KUSHABA; ...I'm Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I, Love You,(Aiyayaaaaa)…I'm Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I Love You,..(Aiyayaaaaa)..I'm Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I Love You, (Aiyayaaaaa)..I'm Going Koo Koo, Na Sijishuku I, I Love You.
Hashim Donode akipiga vocal kwa hisia kali mpaka mishipa ya damu ikimsimama kichwani, hii yote ni kuhakikisha mashabiki wa Skylight Band wanapa ladha ya kitu roho inapenda.
nakupenda pia pia aha....Nakupenda pia...You make me wanna say....Nakupenda pia pia ahaa......Kolabo ya UTAKE matata sana inayowabamba mashabiki wa Skylight Band kati ya Bela Kombo na Hashim Dononde huku wakisindikizwa na Digna Mbepera.
Mkongwe wa muziki wa dansi Joniko Flower akiwapigishwa ligwaride Sony Masamba, Aneth Kushaba pamoja na Sam Mapenzi Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
mdogo mdogo twende kazi sasa....Majembe ya Skylight Band yakiwajibika jukwaani.
Shabiki alipoamua kupanda jukwaani nakuoyesha ufundi wake wa kucheza nyimbo ya "SHAKE BODY" aliyokuwa akiporomosha Sam Mapenzi.
Pale wapenzi wa Skylight Band wanapokunwa na nyimbo hivi ndio muonekano wao mwingine kama analia, mwingine kashika moyo, mwingine kashika kichwa basi raha tupu tukutane leo jioni Thai Village.
Oya shake body...Oya move body...Make you ring alarm o....Oya shake body burudani na iendeleeeeeeee!
Hashim Donode aliposhuka jukwaa na kuwafuata mashabiki wa Skylight Band na kucheza nao Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Aicha, Aicha, écoute-moi...Aicha, Aicha, t'en va pas..Aicha, Aicha, regarde-moi...Aicha, Aicha, réponds-moi...Si mwingine ni Hashim Donode akikonga nyoyo za mashabiki wa Skylight Band, njoo leo ushuhudie nyimbo mbalimbali kutoka Skylight Band.
Hashim Donode wa Skylight Band akimwimbia mtoto mzuri aliyenogewa na uimbaji wake.
Pichani juu na chini burudani ikiendelea huku wapenzi wa Skylight Band mdogo mdogo wakijisogeza kwenye dancing floor.
Kutoka kushoto ni Mkongwe wa muziki wa dansi Joniko Flower, Aneth Kushaba AK47 a.k.a KOMANDO KIPENSI, Sam Mapenzi pamoja na Sony Masamba wakipiga mavocal ndani ya kiota cha Thai Village Ijumaa iliyopita.
Mashabiki wakijiachia na sebene kutoka Skylight Band.
Bela Kombo akiongoza mashambulizi jukwaani huku Aneth Kushaba na Hashim Donode wakicheza swagga za KIDUKU.
Le Manager her self Aneth Kushaba AK47 na vijana wake Bela Kombo na Hashim Donode.
Bela Kombo na Digna Mbepera wakipata Ukodak.
0 comments:
Post a Comment