Tukiachana na mambo ya maskendo, kumbe mwanadada Rihanna anajali sana ubinadamu. Rihanna anamiliki kituo cha misaada ambacho amekipa jina la bibi na babu yake Clara Lionel Foundation.
Usiku wa Alhamisi iliyopita Rihanna aliitsha party ya Diamond Ball jijini Los Angeles kwa ajili ya kuchangisha fedha ambazo zitatumika katika kutoa misaada kwa lengo la kuboresha maisha ya jamii katika nyanja ya afya, elimu, sanaa, na utamaduni kupitia Clara Lionel Foundation.
Mastaa kibao walikuwemo ndani kusapoti ishu hiyo ya Riri. Mastaa kama Brad Pitt, Kim Kadarshian na mkongwe Fabulous walionekana kuanzia red carpet.
Fabulous |
0 comments:
Post a Comment