Miss South Africa 2014 ndiye amewapiga chini warembo 121 kutoka mataifa 121 duniani. Mrembo Rolene Strauss mwenye umri wa miaka 22 ndiye amevishwa kilemba cha miss world 2014 na kuwatupa kule wapinzani kutoka Hungary (Edina Kulcsar) na U.S.A ( Elizabeth Safrit).
Mashindano hayo ambayo yamefanyika jijini London Uingereza yameshuhudia Rolene ambaye pia ni mwanachuo wa mwaka wa nne akisomea utabibu ( medicine) akiitoa kimasomaso Afrika kusini na Afrika kwa ujumla kwa kuipa taji la mrembo wa dunia kwa mwaka 2014.
Warembo wakichuana katika fainali ya Miss World 2014 |
0 comments:
Post a Comment