Ben Haenow aibuka mshindi X Factor 2014

Mdau wa burudani sitaki upitwe na hii ya X Factor. Shindano kubwa la kusaka vipaji vya muziki dunniani limefikia mwisho kwa mwaka 2014 leo huku mwimbaji wa Croydon Ben Haenow akiibuka kidedea.
 
Fainali imefanyika usiku wa Jumapili hii na mwimbaji huyo wa Man in the Mirror ya Michael Jackson amempiga chini mpinzani wake Fleur East.
"Siamini! siamini!" Haenaow alizungumza kwa furaha baada ya MC Dermot O'Leary kumtangaza kama mshindi. "Asanteni sana kwa kuzifanya ndoto zangu kuwa kweli"
Katika fainali hii ya  X Factor  2014 mashabiki wamevunja rekodi kwa kupiga jumla ya kura milioni 40 rekodi ambayo haijawahi kutokea katika mashindano hayo.
Flaeur alionyesha ushindani kwa kuimba "Uptown Funk" wa Mark Ronson akimshirikisha Bruno Mars.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment