KOCHA MNYARWANDA ALIYETAKIWA NA SIMBA AFARIKI DUNIA



Kocha maarufu nchini Rwanda, Jean Marie Ntagwabila amefariki dunia.

Ntagwabila alizidiwa kete kidogo na Goran Kopunovic ambaye ndiye kocha mkuu wa sasa wa Simba.
Wawili hao ndiyo waliingia fainali katika kuwania kuinoa Simba kuchukua nafasi ya Mzambia,
Patrick Phiri.
Habari kutoka Rwanda zimeeleza, kocha huyo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu.
“Kweli kocha hatuko naye tena, amefariki dunia kwenye Hospitali ya Kanombe inayomilikiwa na jeshi,” alisema mmoja wa wanahabari wakongwe wa Rwanda, Clever Kazungu.
Ntagwabila aliyewahi kung’ara na APR akiwa mchezaji na baadaye kocha, pia alizifundisha kwa mafanikio makubwa Atraco, Rayon na Kiyovu.
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment