Siku ya jana ilikuwani siku ya kuzaliwa ya mwanadada Esma ambae ni dada wa msanii mkubwa wa Bongo Fleva hapa nchini, Diamond Platnumz. Kama unavyojua tena mambo mitandaoni
Alianza mwanadada Zari, ambae ni mpenzi wa sasa wa Diamond, kumtumia Esma ujume wa kumtakia furaha kwenye siku yake ya kuzaliwa na kumuita Esma kama WIFI. Watu wakaichukulia poa kwani ni kweli wifi yake.
“Happy bday to my lovely wifi @esmaplatnum. Love you doll”-Aliandika Zari na kuweka picha ya Esma
Baada ya saa moja kupita,mwanadada Wema ambae alikuwa mpenzi wa Diamond nae aliibuka na kutupia, na ujumbe mzito wa kumtakia Esma furaha ya siku yake ya kuzaliwa na kumuita MKWE.
“Happy Birthday to you my Gorgeous Mkwe.... Nakupenda juzi, jana, leo na kesho.... Si unajua vile tupo na ma Loveee ya ukweli kabisa.... Basi God grant u happiness honey on this special day ya kwako.... @esmaplatnum”-Wema aliandika na kuweka picha hiyo hapo juu akiwa na Esma
Kitendo hiki kilizua mjadali mkubwa sana mitandaoni, wapo waliosema Wema kama amejibu hivi kile alichoandika Zari, kwani angeweza kuandika na bila kumuita hata jina lake na sio MKWE kwani sio kweli kwamba huyo ni mkwe wake, na wapo wengine waliosema ni sawa kwani, Esma ameolewa na mfanyakazi wa Wema kwenye kampuni yake ya Endless Fame, Petti Man.
0 comments:
Post a Comment