Msanii maarufu wa filamu kutoka Ghana Van Vicker ambaye alijipatia umaarfu kupitia filamu zake nyingi alizocheza amejiingiza rasmi kwenye soko la muziki. Akiongea na Ghana Vibes, Van Vicker amesema ameshafanya mengi mazuri katika soko la filamu akiwa kama muongozaji (director), mtayarishaji (producer) na muigizaji (actor), hivyo ni wakati wake sasa kugeukia soko la muziki hususani soko la kimataifa la muziki. Hivi karibuni msanii Van Vicker alifanya filamu na msanii kutoka tanzania Wema Sepetu filamu iitwayo Day after Death ambayo mpaka sasa bado aijatoka.
Vack Vicker akiwa na Wema Sepetu |
0 comments:
Post a Comment