Miongoni
mwa stori zilizochukua headline kwenye radio mbalimbali, hata kwenye
magazeti ni kuhusiana na msanii wa Ommy Dimpoz kuzuiliwa kuingia
Marekani na kurudishwa Tanzania bila kufanya show zake.
Sasa
basi Kupitia Amplifaya ya Clouds FM Ommy Dimpoz ame amplify na
kusema;”…Mimi hata mwenye hizo habari zimenishangaza na
kilichonishangaza zaidi stori jinsi zilivyokuja na zilizovumishwa sijui
zimekuja vipi kimenishangaza zaidi au unakuta hata mtu ni professional,
watangazaji, Waandishi,wengine mtu aandika tu stori au anaongelea stori
kwa maana unatengeneza stori kwa kusikia kitu ambacho hauna ushahidi
wala haujamsikia mhusika pengine hata kuongea na management yangu, au
lakini hata kuongelea ile kuhusu mhusika maana meneja wangu aliniambia
ameulizwa imekuaje akawajibu kwamba Ommy ame ni text anarudi leo kwa
hiyo yeye atakuwa na majibu yote lakini unakuta stori tu zinaongelewa
ambapo hata mimi mwenyewe sijasikilizwa kitu gani kimetokea..”
Millardayo….. Ilikuwaje?
Ommy
Dimpoz:…”kilichotokea ni kwamba mimi nilitoka hapa nikaenda mpaka
Amsterdam na Amsterdam nilikuwa na connect flight kutoka Amsterdam
kwenda detroit na detroit kwenda Vegas kwahiyo kufika Amsterdam nilimiss
flight ya connect Amsterdam kwenda detroit kwa hiyo ikabidi ni rebook
booking yangu ili nipate flight nyingine ya kwenda Las Vegas kwa hiyo
nikakosa connection ya kwenda detroit nikapata connection nyingine ya
kupitia Minnesota nilivyofika kule wakati nimefika airport ndege ambayo
nilipata connection na hii ya pili ikawa tayari ilikuwa imenichelewesha
kwasababu ilikuwa inatakiwa inifikishe siku ya show sasa pale kukawa na
tatizo kule watu wa venue siku ambayo waliokuwa wameongea nao
kwa
hiyo ikabidi waongee kuwa msanii amechelewa lakini tunaomba event
tufanye siku nyingine lakini wale jamaa wakakataa wakasema haiwezekani
na lengo ilikuwa mimi ni perform kwenye hiyo weekend ya ruby kwa hiyo
kutokana na mazingira hayo ikabidi wale watu wa immigration unajua siku
zote ukifika ile ni nchi unavyoingia siku zote lazima kuna maswali ya
security pale lazima uulizwe, unajua watu hawajui kitu kimoja kwamba
kupata visa sio ndio kuingia kwenye nchi ya mtu kwamba ukifika nchi
yoyote hata sisi tunaenda South Africa naona ni nchi ambayo tunaingia
bila visa ukifika airport lazima uulizwe unakuja kufanya nini, unakaa
siku ngapi, kwa hiyo nchi zote utaratibu ndio huo kwa hiyo katika pale
kuulizwa nikawambia naenda Las Vegas kwenye show, kwa hiyo mara nyingi
unajua wa marekani ni watu wakutaka kujiridhisha au hata hapa Tanzania
wageni wanakuja unaweza ukamuona Mzungu, Mhindi, Mwarabu, mtu mweusi
akifika pale kwenye passport control lazima wahusika wa hapo airport
wajiridhishe pengine hata wapige simu kwa huyo mwenyeji wako, kwahiyo
wakapiga simu kule kwa watu wa event pamoja na sehemu ya Venue kwa hiyo
watu wa Venue wakaambiwa kulitakiwa kuwe na show ila msanii hakufika kwa
hiyo wakabidi waongee na promote akasema tumeisongeza kwasababu msanii
amechelewa amemiss flight sasa wakarudi kwangu wakaniambia lengo
lilikuwa uje kwenye hii show na show tayari umeshaimiss kwasababu ya
matatizo ambayo sisi hatutakiwa kuyajua yamesababishwa na nini wakasema
kwamba lakini hapa inaonesha una show nyingine New york tarehe 21
nikawaambia ndio nilikuwa ninayo ila nilipanga nikitoka Las Vegas
naelekea huko.
Wakaniambia
sasa hii show ndio tunatatizo nayo kwasababu ni show ambayo inahusisha
chama cha kisiasa na kama uliona hata kwenye promotion yangu nilikuwa
nimeandika kuwa nitakuwa na show ya miaka 38 ya CCM Marekani, unajua
vyama cha siasa hivi Chadema, CCM wanamatawi yao kule Marekani watu
wanaoishi nje mara nyingi uwa wanafanya sherehe sherehe za Annivesary ,
kwa hiyo wakaniambia kuwa hii visa yako haikuruhusu wewe kuperform kuna
aina ya Visa ya inayoruhusu msanii ku perform kwasababu show yako ni
kama ya kisiasa, kwa hiyo kwa kuangalia hivyo wakaniambia option iliyopo
itabidi nirudi nyumbani kwasababu shughuli iliyokuleta imeshindikana
kwa hiyo unaweza ukaja mwenyewe baadae kwa matembezi yako au kwa nini
lakini hata ikitokea mfano leo nikakatiwa ticket au nikate ticket nirudi
Marekani visa yangu sasa hivi hainiruhusu kwa hiyo ina maana ninataka
kuchukue visa nyingine yenye kibali maalumu chenye kuperform mimi kwenye
show, na kama ukivunja sheria zao wanaweza wakakufungia miaka mitano
halafu wanakupiga faini dola elfu 1o kwa hiyo mimi mwenyewe nikakubali
lazima pia uangalie mazingira na mimi lazima nitengeneze mazingira yangu
ya kazi kwa hiyo nikawaambia sawa nitarudi nyumbani kwa hiyo nasubiri
tu sasa hivi wale promote wa show ya Las Vegas wapange kwaajili ya venue
ya show nyingine then nitaendelea na mchakato mwingine kama kawaida.
Millardayo…:
‘ilikuwaje mpaka unamiss Flight?
Ommy Dimpoz: unajua kumiss flight
kunatoka hata hapa Dar unaweza ukamiss flight, unajua nilishazoea kukaa
kwenye zile connection za masaa matatu reporting time kwahiyo
nilijichanganya kwenye masaa halafu ukishaondoka hivi inakuwa kidogo
hivi masaa yanazigua kwa hiyo inabidi uwe makini kidogo kwa hiyo katika
kuangalia pale yaani mimi fikra zangu na mawazo na nilishazoea zile
flight za kuunganisha labda za kwenda DC unaweza ukakaa pale masaa
matatu au masaa matatu na nusu kufanya connection ya kwenda lakini ile
ilikuwa na connection ya muda mfupi kama lisaa limoja kwa hiyo mpaka
ushuke, utoke sijui geti unalotakiwa kwenda kwahiyo katika mishe mishe
nikakuta ile flight mlango umeshafungwa kila kitu wakasema haiwezekani
na hata begi langu walikuwa wamelishusha kitu kingine nimeshazoea kama
mule uwanja unataka watu wanatangaza kwasababu ilishawahi kunitokea mara
nyingine labda unakuta abiria amechelewa flight kwasababu sisikii
tangazo lolote nimekaa angani kama almost masaa tisa nafikiri nane
kutoka Dar kwa hiyo nilipofika nikaunganisha wifi nikawa nimepata
internet nikaingia ghafla kwenye whtsspp nasoma SMS nawaambia washikaji
wa kule marekani kuwa nakuja nimeshafika Amsterdam kitendo cha pale
kuchati kuwa wish watu valentine nakutana flight imeshaondoka.
Millardayo…: ‘Baada ya wao sasa kukuambia unarudi Tanzania yaani uligeuzia pale pale Airport au mazingira yalikuwaje?..
Ommy
Dimpoz…;“Waliniweka Hotel kwa sababu hiyo flight ilikuwa ni ya siku
inayofata ambayo ni jioni mpaka zile ndege zinavyotoka huku zifike
Amsterdam, zifike pale kwa hiyo ilikua ni siku inayofata.
CHANZO-millardayo
0 comments:
Post a Comment