Jide
akiwa na Mokonyo (mtoto wa mdogo wake Dabo)Lady Jaydee ameendelea
kujibu maswali ya mashabiki wake kupitia Instagram, na maswali mengine
aliyokutana nayo ni kuhusu kama ana mtoto au ameasili mtoto ambaye
huonekana kwenye kipindi chake cha ‘Diary Ya LadyJaydee’ kinachorushwa
kupitia EATV.
“SWALI: Una watoto wangapi?
JIBU : Sina mtoto wala watoto
SWALI:Utazaa lini?
JIBU : Sijajua mpk sasa nitazaa lini, ila siku yoyote ile ikitokea naweza kuzaa
SWALI: Kwanini huna mtoto /watoto?
JIBU : Sina mtoto /watoto sababu sijawapata, nikipata nitakuwa nao.
SWALI: Tunaskia ume adopt mtoto ?Na mtoto tunaekuona nae ni wa nani?
JIBU :
Sija adopt mtoto, mtoto mnae muona ana shine like a star, ananiita
Shangazi, ninaishi nae sbb ya ukaribu wa shule anayosoma ,Tunaishi
wawili tu, mimi na yeyeAnaitwa “Mokonyo Yvonne Mbibo” Ni binti wa mdogo
wangu @dabomtanzania
SWALI: Tunaskia una mtoto mkubwa ulimzaa ukamuacha kijijini Shinyanga /Musoma
JIBU : Sina mtoto niliemuacha
kijijini, sijawahi kuishi kijijini.Sijawahi kuishi Musoma, kwetu ni
Bunda na huwa naenda ikitokea misiba kuzika, sijawahi kuishi huko zaidi
hata ya miezi 2 Shinyanga niliozaliwa ni mjiniNilihama Shinyanga, kuja
Dar es salaam nikiwa na miaka 11Sijawahi kurudi kuishi huko tena zaidi
ya kwenda kusalimia.
SWALI: Tunaskia huzai, ulitoa kizazi ili ufanikiwe kifedha?JIBU : Sijatoa kizazi na sifanyi kitu chochote unusual ili kupata mafanikioAngalizo : Mwenyezi Mungu hadhihakiwi, so stop calling me names. …….Kesho anaijua yeye, lolote pia linaweza kutokea. Accept me the way I am”.
0 comments:
Post a Comment