Aliyekuwa mpenzi wa rapper Nay wa Mitego, Siwema ameamua kuonesha jeuri ya pesa kwa kununua gari mpya ya kutembelea. Mkoko mpya wa aliyekuwa mpenzi wa NaySiwema ambaye ni mama wa mtoto mmoja na Nay, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameshare na mashabiki ndinga yake mpya ikiwa ni wiki tatu tu tangu waachane na rapper huyo.“Thank u ZAMZAM MOTORS LTD…..kwakufanikisha hili…u always good to me#magari yenu yako bomba ile mbayaaa # namba ikitoka ntawambia ili msinipite barabarani,” ameandika Siwema kwenye picha hiyo.Hivi karibuni Nay na Siwema waliachana na kurushiana maneno mtandaoni ambapo Siwema alidai kuwa mtoto aliyezaa si wa rapper huyo.
|
0 comments:
Post a Comment