Busu la Lady Madona kwa Drake lazua kizaizai mitandaoni.
Ni katika usiku wa kuamkia leo (usiku wa tarehe 12 Aprili) ambapo rapa Drake aliungana na maelfu ya wapenda burudani waliokuwa ndani ya Coachella kustaajabu ya Musa. Mwanamuziki nguli Lady Madonna alimtwanga rapa huyo busu la nguvu Drake wakati akiwa jukwaani. Rapa huyo mwenye asili ya Canada alikuwa moja ya Waburudishaji wakuu katika jukwaa la Coachella huko California na alipatwa na butwaa baada ya Malkia wa muziki wa Pop, Lady Madona kumfuata alipokuwa ameketi jukwaani akamuinamisha kichwa kwa nyuma kisha kumpa busu ambalo lilichukua sekunde kadhaa.
Madonna alifanya kitendo hicho baada ya kutumbuiza kama mgeni katika tamasha hilo kwa kibao chake ambacho kimewahi kusumbua vilivyo "Human Nature".
Baada ya kupata busu hilo Drake hakuamini kilichotokea na alicheka huku akiwa ameshika mdomo huku Madonna akiondoka stejini akijisemea "Mimi ndiye Madonn".
Wakati akifanya hayo wahudhuriaji waliwasha moto wa kelele zilizofanya siku hiyo kuwa murua. Ni mchanganyiko wa kijana wa miaka 28 (Drake) na miaka 56 (Madonna).
0 comments:
Post a Comment