Diamond Platnumz: Ilikuwa ni lazima tuachane na Wema Sepetu ili maisha mengine yaendelee


Star wa Bongo flava Naseeb Abdul Jumaa “Diamond Platnumz”, amesema kuwa ilibidi aachane na Wema Sepetu ili maisha mengine yaendelee.
zari-diamond4Kupitia mitikisiko ya pwani Times Fm, Diamond amedai mara kadhaa alitumia nguvu nyingi kujenga mahusiano yake bila mafanikio, kwa kuwa yeye na Wema “Madame” hawakuendana tabia.
“Nafikiri hatukuendana tabia kwa kuwa nilifanya kila niwezalo, tulikubaliana kwa pamoja na ikafika hatua ikawa ni lazima tuachane tu” alifunguka Chibu “Diamond”.
Kwenye line nyingine Plutnumz alithibithibitisha rasmi ujauzito wa kichuna wake wa sasa Zarrina Hassan “Zarri the boss lady”, na kumpa sifa mob kuwa ni mwanamke wa pekee aliyekubali kupata nae mtoto.
“Mabinti wengi niliokua nao, na hata wa hapa mjini kukubali kua na mtoto ni jambo zito sana so nina kila sababu ya kumshukuru sana na nampenda kwa kweli,” alimalizia Diamond.


Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment