JUSTIN BIEBER SASA MCHUMBA WA KUOA


Staa wa muziki wa Pop nchini marekani, Justin Bieber.
New York,Marekani
UNAWEZA kusema sasa Justin Bieber amekuwa hii ni baada ya kutamka wazi kuwa anahitaji mwanamke ambaye anajiamini na mwaminifu ili aweza kuishi naye katika maisha yake baadaye.
Justin Bieber akiwa na rafiki yake Jayde Pierce.
Hii ni kutokana na star huyo kuwa karibu na mwamitindo Jayde Pierce (19)  ambaye hivi karibuni  wamekuwa wakiongozana na haifahamiki kama ni wapenzi au la. Japo hakuna aliyeweka wazi uhusiano huo lakini inaelezwa kuwa wawili hao wamekuwa wakikutwa sehemu mbalimbali pamoja ikiwemo kwenye migahawa.
Kabla ya kuwa na Jayde, Bieber alikuwa akihusishwa kutoka na Haley Baldwin baada ya kuachana na mpenzi wake wa awali Selena Gomez.“ Nahitaji mtu ambaye anajiamini na mwaminifu, nahitaji kutafuta msichana anayevutia na ambaye atakuwa na mimi maisha yangu yote. “ Nataka  uhusiano salama na  watu wasiweze kunizungumzia,”
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment