MAPENZI YA RONALDO NA ALESSIE YANOGA


Mshambuliaji wa Real Madrid ,Cristiano Ronaldo.
Madrid, Hispania
KUMEKUWA na taarifa kuwa  mshambuliaji wa Real Madrid ,Cristiano Ronaldo, ambaye hivi karibuni amevunja rekodi yake mwenye kwa kufunga mabao 61 kwenye La Liga, anatoka na Mwigizaji na Mwanamitindo Alessia Tedeschi.
Mwigizaji na Mwanamitindo Alessia Tedeschi.
Ronaldo hivi karibuni aliachana na aliyekuwa mpenzi wake Irina Shayk lakini bado hajafunguka hadharani kuhusu uhusiano huo mpya. Inadaiwa kuwa  mwanadada Alessia, alifunga safari kutoka Italia mpaka Hispania kwenda kumuangalia Ronaldo wakati Madrid ilipokuwa ikivaana na Juventus kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya nusu fainali.
Tedeschi alikutana na Ronaldo kupitia  kampeni ya ‘Arman Exachange’ kama mwanamitindo na baada ya hapo ndipo wakaanza uhusiano wa kimapenzi.
Tedeschi, inaelezwa kuwa amekuwa akiweka picha za staa huyo ambaye anashikilia tuzo ya mchezo bora wa dunia kila mara kwenye mtandao wake wa Instagram na mashabiki wake kuhoji mara kwa mara kuhusu uhusiano huo.
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment