MwanaFA amesema kuwa Staa wa Bongo,Diamond ana haki ya kutoa maoni na malalamiko yake kuhusu tuzo za muziki za Kilimanjaro(KTMA) za mwaka huu.
Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena,alisema kilichomtokea Diamond hata yeye kilimtokea wakati alipotoa wimbo wake wa ‘Bado Nipo Nipo Kwanza’ ulifanya vizuri wakati huo lakini jina lake halikuwepo kwenye tuzo hizo. ‘’Hata mimi nililalamika kama anavyolalamika Diamond lakini niliwaandikia barua Killi wakaniita wakanielewesha kuwa ilikuwa ni makosa ya kibinadamu nikaelewa,’alisema Mwana FA.
Pamoja na hayo MwanaFA amesema amesikitishwa na wasanii kama Mo Music na Ommy Dimpoz kutokuwepo kwenye tuzo hizo hasa video ya ngoma ya Ndagushima ambayo ilifanya vizuri mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment