Diamond Platinumz ameachia video ya wimbo wake mpya aliomshirikisha Msanii kutoka Nigeria, Mr. Flavour. Wimbo huo ambao umeachiwa rasmi jana unakwenda kwa jina la "Nana" .
Mpaka kufikia sasa tayari watu 110,459 wamekwisha kuutazama wimbo huo kupitia akaunti ya You Tube ya mfalme huyo wa Muziki wa Kitanzania anayechanja mbuga kwenda kimataifa.
Video hii imetengenezwa na God Father Production kutoka Afrika ya kusini wakati ala ya wimbo huo ikitengenezwa na mzalishaji wa muziki kutoka hapa nyumbani, Nahreel na mashairi kuandikwa na Diamond kwa kushirikiana na Mr. Flavour.
"Nana" ya Diamond na Mr. Flavour iko hapa.
12:01 PM
BET
,
BONGO FLEVA
,
Diamond Platnumz
,
God Father
,
MASTAA MUZIKI
,
Mr. Flavour
,
Nahreel
,
NEW VIDEO
Edit
0 comments:
Post a Comment