Nay wa Mitego akipozi na Mtangazaji wa Kipindi cha Sporah.
STAA wa Bongo Fleva nchini, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuhusu mali zake anazomiliki.
Nay ameyafunguka hayo wakati akihojiwa katika Kipindi cha Sporahkinachoruka kupitia Runinga ya Clouds TV kila Jumanne usiku.
Nay wa Mitego akipozi na Mtangazaji wa Kipindi cha Sporah.
Staa huyo amesema anamiliki nyumba tatu, magari matatu ambayo ni Toyota Prado, Nissani Murano na Toyota Passo.
Mbali ya vitu hivyo pamoja na muziki, pia staa huyo anavitega uchumi ambavyo vinamuingizia kipato ikiwemo bajaj, saluni na vinginevyo.
Mojawapo ya mijengo ya Nay.
Kwa upande wa mahusiano, Nay amesema kwa sasa yupo ‘single’ akiwalea watoto wake wawili baada ya kutofautiana na mpenzi wake wa tatu Siwema na kuamua kumchukua mtoto wake mchanga anayedai alikuwa hapati malezi bora kutokana na mama yake huyo kuwa bize na biashara zake.
Nay akipozi jirani ya mojawapo ya ndinga zake.
Nay ameeleza historia ya mahusiano yake akiweka wazi wapenzi wake watatu ambao amezaa nao watoto akianza na wa kwanza ambaye alikuwa Mhindi huku wa pili akiwa msanii wa sinema za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ kabla ya kumaliza na Siwema ambaye wametofautiana hivi karibuni.
Nay wa Mitego akiwa na Siwema.
Nay amesema kwa sasa ana watoto watatu ambao aliwapata na wapenzi wake hao watatu wa zamani na kati ya hao wawili anaishi nao.
Lakini mbali na kusema kwa sasa yupo single, staa huyo hivi karibuni amekuwa na uhusiano wa karibu sana na mwigizaji wa filamu za Kibongo Shamsa Fordhuku wakipiga picha kadhaa za kimahaba na kuziachia mitandaoni.
Nay na Shamsa.
Kuhusu muziki, Nay amefunguka kuwa yeye anafanya muziki biashara akiangalia soko la muziki linataka nini ili aweze kuendelea kuwa juu.
Nay akiwa na mtoto wake aliyezaa na Skyner.
Mipango yake katika miziki ni pamoja na kufanya kolabo mbalimbali na mastaa wa nje akiwemo Wizkid na D’banj na wengineo ambapo baadhi yao tayari amenza kufanya nao kazi.
Nay akiwa na mwanaye aliyezaa na Siwema.
Kwa upande wa hapa Bongo, Nay amesema anatarajia kutoa ngoma nyingine ambayo amefanya na mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz huku akiongeza kuwa atafanya pia kolabo na wasanii wa kike ili kuboresha muziki wake na kuwapa raha mashabiki wake.
CHANZO; GPL
0 comments:
Post a Comment