Rihanna aanza kufanya kweli kwenye matangazo ya Dior
Siku chache baada ya mrembo mwenye kipaji kikubwa cha muziki, Rihanna kuvunja rekodi kwa kuwa mtu mweusi wa kwanza kuteuliwa kuwa balozi wa Jumba la Mitindo la Dior lililoko nchini Ufaransa, tayari mkali huyo wa "Four Five seconds" ameanza kampeni za matangazo.
Picha za matangazo ya Dior ambazo zimepambwa na mlimbwende huyo raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 27 zimeanza kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii na kuifunika ile ya vazi alilovaa katika sherehe za Met Gala.
Rihanna ameonekana kukolea katika fasheni kwani hata Mkurugenzi Mkuu wa Dior wakati akihojiwa na WWD alimsifia Rihanna kwa kusema "Rihanna ana mwonekano mzuri na tuliliona hilo toka mwanzoni, anaweza kushangaza. Ana uwezo wa kuwa vile ambavyo haikutarajiwa na ni sehemu ya mwonekano huu"
Zitazame hapa picha ambazo zimepigwa katia viunga vya Varseil huko Ufaransa tayari kwa kuanza kampeni ya matangazo ya Dior.
0 comments:
Post a Comment