Hatma ya Mario Baloteli katika klabu yake ya Liverpool imezidi kugubikwa na utata hasa baada ya kusajiliwa kwa mshambuliaji Christian Benteke ambaye anaonekana kuwa chaguo la kwanza kwa kocha Brendan Rogers.
Hata hivyo mshambuliaji huyo mwenye sifa ya utukutu anaweza kuendelea kubaki kunako Ligi Kuu ya Uingereza na klabu ya Liverpool endapo Manchester United wataifunga na kuito klabu ya Lazio katika mtoano wa kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa Ulaya. Klabu hiyo ya Italia imepanga kumchukua Baloteli kwa mkopo endapo itafuzu hatua ya mtoano kwenda kwenye makundi kucheza klabu bingwa Ulaya (UEFA).
0 comments:
Post a Comment