SBL yazindua kampeni ya ‘Usitumie Kilevi na Kuendesha Chombo cha Moto’ mkoani Tanga

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kampeni inayolenga kutoa elimu kwa umma juu ya unywaji wa kistaarabu, ikiwa ni moja ya hatua muhimu inayochukuliwa na kampuni hiyo kuzuia ajali nyingi zinazosababishwa na madereva wanaoendesha wakiwa wametumia vilevi

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Tanga, Solomon Mwangamilo, akimvalisha reflector mmoja wa madereva wa pikipiki (bodaboda) katika tukio la uzinduzi wa kampeni ya ‘Don’t Drink and Drive’ inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti ikiwa na lengo la kutokomeza ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva walevi.
Kampeni hiyo inayobeba ujumbe wa, “Usitumie Kilevi na Kuendesha Chombo cha Moto’ imezinduliwa jijini Tanga leo katika Stendi ya mabasi na kuwakutanisha pamoja wadau mbalimbali ikiwamo Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, madereva, abiria, na wadau wengine katika sekta ya usafirishaji

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) Tanga, Solomon Mwangamilo, amesema kwa kulishirikisha jeshi la Polisi kampuni ya SBL imeiunga mkono serikali katika kuelimisha umma juu ya unywaji wa kistaarabu na kusisitiza umuhimu wa kutatua tatizo hilo.

RTO amesema baadhi ya watu na haswa madereva hunywa kiasi kikubwa cha pombe pasipo kujali madhara yanayoweza kusababishwa na kitendo hicho na kuonya kuwa vitendo vya aina hiyo vinaweza kusababisha ajali mbaya barabarani.

“Sote tunafahamu kuwa matumizi ya vileo yana uhusiano mkubwa na uendeshaji mmbovu ambao unaweza husababisha ajali mbaya za barabarani zenye athari kubwa kwa jamii zetu. Athari zake siyo tu zinawagusa watumiaji wa vilevi bali hata maisha ya wengine na kusababisha upotevu wa maisha na ulemavu kwa watu ambao wangeweza kuchangia uchumi wa nchi,” amesema.

RTO ameongeza kusema kuwa pamoja na kusababisha vifo visivyotarajiwa na majeraha, unywaji usiokuwa wa kistaarabu una maadhara makubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwa kiasi kikubwa cha fedha kinatumika kwa ajili ya huduma, madawa na vifaa tiba kwa waathirika wa ajali za barabarani na hivyo kuwa ni mzigo kwa Serikali.

Akizungumzia namna kampeni hiyo itakavyoisadia jamii, mkuu huyo wa usalama barabarani amesema, “sote kwa pamoja ikiwamo askari, madereva, jamii na wadau wengine tuna jumuku la kutafuta suluhisho la kumaliza tatizo la kutumia vilevi na kuendesha vyombo vya moto. Ninayo furaha kuona SBL pamoja na kwamba biashara yao ni kuuza vilevi, wameona wanawajibu wa kuhimiza unywaji wa kistarabu”. 

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL John Wanyancha amesema kampeni ya unywaji wea kistaarabu inalenga kuielimisha jamii kuwa wanywaji wanapaswa kunywa kwa kiasi na kuhakikisha unywaji wao hauna madhara kwao na kwa watu wanaowazunguka. 

“SBL imedhamiria kuungana na serikali na wadau wengine kuhakikisha kuwa jamii na haswa madereva ambao wanakunywa na kuendesha vyombo vya moto wanaelimishwa juu ya madhara ya vitendo hivyo na kutakiwa kubadilisha tabia,” amesema Wanyancha. 

Kampeni hii ambayo imekuwa ikifanyika katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania, inalenga kuwafikia vijana na watu wengine kwa kuwaeliisha juu ya madhara ya unywaji usiokuwa wa kistaarabu huku ikiwataka kubadili tabia kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla. 



Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments:

  1. Best Casino Deals in Palm Springs - MapYRO
    강릉 출장샵 miam-parks › 경주 출장마사지 las-paf › miam-parks 창원 출장샵 › las-paf This 경상북도 출장안마 beautiful Palm 경주 출장샵 Springs resort offers 4-star accommodation and is located in The Country Club area.

    ReplyDelete