KAMA HUKUTAZAMA MECHI KATI YA MAN U NA REAL MADRID: HAYA HAPA MAGOLI
Jana katika dimba la Michigani huko  Marekani , miamba miwili ya soka ulimwenguni ilivaana. Manchester United wakiongozwa na kocha Van Gaal waliirarua Real Madrid iliyo chini ya kocha Anceloti kwa jumla ya magoli 3-1.
Magoli ya Man U yalifungwa na Ashley Young ambaye aliingia nyavuni mara mbili na Javier Henerndez (Chicharito), huku goli la kufutia machozi la Real Madrid likiwekwa kimiani na Gareth Bale kwa mkwaju wa penati. Ushindi huo umeipa nafasi Man U kucheza fainali ya michuano ya kombe la Mabingwa wa Kimataifa (International Champions Cup) ambapo watavaana na Liverpool
Nimekuwekea video ya magoli yote hapa, ili mdau wangu ujionee mwenyewe:

Pia mchezo huo uliopigwa katiak uwanja wa Michigani ulivunja rekodi kwa kuingiza idadi kubwa ya mashabiki wapatao 109, 000 na kuifunika rekodi ya michuano ya Olimpiki ya mwaka 1984 ambayo ilishuhudia mashabiki 101,799 wakiingia katika dimba la Rose Bowl huko Pasadena, California kushuhudia mchezo wa fainali kati ya Brazil na Ufaransa.

Manchester United - Real Madrid smashes attendance record in USA
Share on Google Plus

About Mallya Michael

Born in Moshi ,live i Tanga, studied in Arusha, went for military training at Kanembwa in Kigoma & currently pursuing my B.A in Public Relations & Advertising in University of Dar es Salaam
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment