50 CENT NA SAKATA LA KUFUNGIWA AKAUNTI YA BENKI

Mkali wa Miondoko ya Hip Hop, Curtis James Jackson III maarufu zaidi kama 50 Cent amepata mkasa wa kufungiwa akaunt yake ya benki baada ya kupinga maamuzi ya mahakama ya kuilipa dola za kimarekani milioni 17 kwa kampuni ya Sleek Audio.
  50 Cent's Bank Account Frozen Due To Sleek Lawsuit
 Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Aprili mwaka huu 50 Cent aliamuriwa na mahakama kuilipa kampuni ya Sleek Audio kiwango cha dola milioni 17 baada ya kushindwa kesi iliyofunguliwa na kmpuni hiyo dhidi yake. Sleek ilimfungulia kesi 50 Cent baada ya kiongozi huyo wa G Unit kukiuka makubaliano waliyofanya ya kushirikiana kutengeneza headphones. 
50 Cent alikiuka makubaliano aliyofanya na Sleek Audio na baada yake akatumia wazo sawa, akajiunga na kampuni nyingine kutengeneza headphone zake zinazojulikana kama Sync By 50 headphones.
Mwanasheria wa 50 Cent akizungumzia sakata hilo amekiri kufungiwa kwa akaunti binafsi ya benki ya 50 Cent lakini akakazia kuwa bado watakata rufaa kwa maamuzi yaliyotolewa. 


Ni haki yako msomaji wangu kupata habari za kipekee kama hizi, like facebook page ya Mwanaharakati uwe mjanja zidi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment