Vanessa Mdee azungumzia jinsi tuzo 3 za Diamond zilivyowaogopesha wanaigeria

 http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/09/Vanessa-Mdee-mtangazaji-wa-Dume-Challenge.jpg
Akiongea kwenye mahojiano na Bongo5, Vanessa amesema ushindi wa Diamond kwenye tuzo za Channel O ulikuwa mkubwa kiasi cha kuwaogopesha wasanii hao na kwamba hawakutarajia ushindi kama huo kutoka kwa msanii wa Tanzania.
“Nilipata bahati ya kukaa siti za mbele kwenye tuzo za Channel O,na nyuma yangu walikuwa wamekaa wasanii wengi wa Kinaijeria. Kila alipokuwa anashinda Chibu tunasimama tunamshangilia, nilikuwa nimekaa na Victoria Kimani na msanii mmoja wa Kenya anaitwa Yvonne Darq, tunasimama tunamshangilia, ni ndugu yetu, ni rafiki yetu na anatutengenezea vitu fulani hivi,” amesema Vanessa.
“Kwenye kusimama kwetu na kushangalia wale watu walikuwa wanaumia fulani hivi. It was so strange, nawatizama nasema ‘jamani najua mmezoea kushinda na ninajua mnaogopa vile ambavyo hamvielewi but just celebrate kwani kuna tatizo gani’. I think they are shocked, at the same time wanajaribu kuelewa what we are doing right and what they are doing well.”
“But kusema ukweli wamefanya vizuri sana wenzetu katika muziki katika this past few years but if you look back, muziki wa Bongo Flava ulikuwa ni mkubwa zaidi na ulikuwa ushadevelop vitu fulani kabla ya Wanaijeria hawaja popular on the African scene so I think it’s time to reclaim the throne.”
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment