Video: Mtazame hapa mrembo anayefananishwa na Rihanna


Usemi wa dunia ni wawili wawili wakati mwingine hudhihirika kuwa kweli. Mwanadada mkali wa Pop, Rihanna amepata mtu ambaye anafananishwa naye zaidi.
Mrembo Andele Lara mwenye miaka 22 ni mwanafunzi anayetokea Boston - Masachuttes, mrembo huyo hawezi kumaliza siku bila kuzongwa na mashabiki au hata wanaume wenye uchu wakidhani ni mwanamuziki Rihanna.
Lara ameliambia Daily Mail kuwa wakati yuko mdogo alikuwa kawaida lakini sasa hivi amepata umaarufu na pesa baada ya watu kuanza kumfananisha na staa huyo wa "Where have You Been".
"Rihanna alipofungiwa Instagram mwezi April baadhi ya watu walinitumia ujumbe mtandaoni wakiniambia nimeziba pengo lake" - alisema Lara.
Aliongeza kuwa "ninapokatiza mitaa watu hawaishi kunizonga na kunipigia kelele na wengi hutaka kupiga picha na mimi. Hii hutokea kila siku, haijalishi nafanya nini.Siwezi kumaliza masaa 24 bila kulisikia jina la Rihanna"
Kwa bahati mbaya Lara na Rihanna hawajawahi kukutana , ingawa amepata wafuasi wengi sana katika akaunti yake ya Instagram ambayo ni @andelelara na kulazimika kuifanya private baada ya baadhi ya mashabiki kuanza kucomment masuala ya Rihanna katika akaunti yake.
Nimetupia video hapa kama kawa akiwa anahojiwa:

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment