Imekuwa
ikielezwa kuwa wasanii ni kioo cha jamii. Kwa maana hiyo wanatakiwa
kufanya mambo ambayo yanaweza kuigwa na wale wanaowatazama. Hata hivyo,
maisha wanayoishi baadhi ya wasanii hayaakisi msemo huo.
Wengi wamekuwa wakikumbwa na skendo mbalimbali zinazowafanya wasiwe na vigezo vya kuitwa kioo cha jamii.
Miongoni
mwa mambo yanayowafanya wakati mwingine wadharaulike ni kutoa maneno
machafu, ‘live’ au kupitia kwenye mitandao ya kijamii.
Staa wa filamu Bongo, Wastara Juma.
Katika
makala haya nitawazungumzia mastaa wanaoongoza kwa kutukana mitandaoni
lakini pia wale ambao wanaongoza kwa kutukanwa katika siku za hivi
karibuni.
Wastara Juma
Huyu
Wastara amekuwa akiheshimika kwenye jamii kwa muda mrefu na alikuwa ni
miongoni mwa mastaa wa kike ambao wangesimama na kuamua jambo
wangesikilizwa kutokana na jinsi alivyokuwa amejiweka na kuwaaminisha
watu.
Lakini
katika siku za hivi karibuni alichafuka kwa kuingia katika orodha ya
mastaa wanaotukana mtandaoni baada ya kumvaa mmoja wa mashabiki wake
aliyemsemea mbovu na kumtukana matusi mazito
“Iweje
anakubali kushushwa na mtu mmoja ambaye alikaa na kuamua kumvuruga,
anasahau kama kuna kundi la watu linamheshimu?” Aliandika mmoja wa
mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram baada ya kuona matusi hayo.
Amanda Posh
Wafuatiliaji
wa mambo na hasa wale ambao wapo Facebook watakumbuka jinsi staa huyu
wa filamu alivyomshambulia jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina la Joel.
Haikuwa
ustaarabu kabisa kwa staa huyo kufanya hivyo kwani jambo
lililomkasirisha angeweza kulipuuza na angebaki na heshima yake huku
yule aliyemtukana akionekana mjinga.
Lakini
ukiacha hilo, Amanda amekuwa akisifika kwa kutoa maneno machafu pale
anapochokozwa, tabia inayomfanya afiti kwenye makala haya.
Msanii wa filamu na muziki, Isabela Mpanda ‘Bela’.
Isabela Mpanda
Katika mastaa micharuko, huyu yumo! Hajivuni, hajisikii lakini ukimchokoza lazima akushikishe adabu kwa matusi.
Posti
zake zenye lugha chafu kwenye mtandao wa Instagram zipo nyingi lakini
pia kwa wale wenye kumbukumbu watakumbuka kuwa staa huyu aliwahi
kumtukana mwanamitindo Belina Mgeni na mpaka sasa hawaongei.
Hao ni baadhi ya mastaa ambao katika siku za hivi karibuni wameshika chati kwenye suala la kutukana mtandaoni.
Kwa upande wa wale ambao wanashika nafasi za juu kwa kutukanwa, wapo wengi lakini leo tutawazungumzia wahanga watatu.
Kajala Masanja: Tangu
aingie kwenye bifu na Wema Sepetu, kuna kundi ambalo linajiita Team
Wema limekuwa likimshambulia kwa kumtukana na kumshutumu kwa mambo
ambayo mengine hayana ukweli.
Hata
hivyo, Kajala anaonekana kuwa mstaarabu kidogo kwani licha ya kutukanwa
mtandaoni, yeye amekuwa mkimya akijua kujibizana na watu hao ambao wala
hawana majina ni sawa na kuzidi kujichafulia.
Elizabeth Michael ‘Lulu’: Huyu
naye ni mhanga wa matusi mtandaoni. Kuna kundi la watu ambao
linaonekana kuwa na chuki dhidi yake, huenda kutokana na mafanikio
aliyonayo akiwa kwenye umri mdogo.
Lakini
sasa, licha ya matusi anayoyaoga mtandaoni, amekuwa mvumilivu wa
kuyaacha yapite. Watu wake wa karibu wanaeleza kuwa, licha ya kutukana
sana mwenyewe wala hajui kwamba anatukanwa kwani si mtu wa kufuatilia
nani kasema nini kibaya juu yake
Wema Sepetu:
Kama
ilivyo kwa Kajala, huyu naye anashambuliwa sana na Team Kajala. Hawa ni
watu ambao wamejitenga kuhakikisha wanamkosesha amani staa huyu.
Amekuwa akitukanwa kwa mengi lakini kwa kuwa anajua ustaa ni kama jalala, huwa hajali na anachukulia poa.
Ni mara chache sana amekuwa akinyanyua mdomo wake kuwajibu wale ambao wamekuwa wakimsema vibaya sambamba na kumtukana.
Kwa uchache hao ndiyo mastaa ambao hivi karibuni wametia fora kwa
kutukana na kutukanwa mtandaoni.
Tahadhari
Mastaa
ambao ni wepesi kutukana mtandaoni wajue kwamba endapo Rais wa Jamhuri
ya Muungano, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete atasaini ile sheria ya makosa
ya mtandaoni ya mwaka 2015, watajikuta wanaenda jela hivi hivi.
CHANZO; GPL
|
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment